“PENZI LA SHEMEJI” SEHEMU YA NNE (4)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Tuliendelea kupiga stor mbili tatu pale na kutaniana mpaka muda wa chakula ulipoisha kila mmoja akaaga na kuondoka kwenda kulala. Usingizi usiku ulikosa kutokana na yale maneno ya shemeji. Nilielewa kabisa yule kuku wa kienyeji aliyekuwa anamuongelea pale ni mimi,nilishindwa kuelewa kula alikuwa na maana gani kumwambia kaka juu ya lile. Nilianza kuogopa kuwa endapo kaka atatambua juu ya maaana halisi ya kuku wa kienyeji anaweza kuniua " 
Na ikitokea nikaja kugundulika kwenye jamii kuwa nilitembea na mke wa kaka jamii itanichukulia vip? Na wazazi je?" niliendelea kuumiza kichwa juu ya lile swala Nilikuja kupitiwa na usingizi muda ukiwa umeenda sana. Kesho yake nilichelewa kuamka kwa sababu ya kuchelewa kulala usiku wa jana yake. Nilipoamka nilikuta kaka na shemeji walishaondoka kuelekea kwenye kazi na biashara zao Nilienda na kupewa chai na yule beki tatu kisha nikaingia kuoga na kuelekea town Nilifika kazin ( nilikuwa nafanya kazi pamoja na shemeji kwenye duka kubwa la kuuza simu za jumla alilofungua kaka kama moja ya kitega uchumi) " 
Waoooh! Handsome wetu umekuja?" alisema shemeji Cha ajabu kaka alikuwepo ila shem hakuogopa kuongea hayo " Dogo vip? Unaona mpaka shemeji yako amekwambia leo ukweli,wewe ni hb yaan basi 2 unajiaachia,anza kujipenda dogo" akasema kaka " Umeona baby,mi namwambiaga pia aanze kujitengeneza mbona mji mzima watamtambua dogo uko poa sana" akasema shemeji Nilikubali kwa shingo upande zile sifa zao " 

Ila jaman sipendi mnavyoniongelesha mambo hayo ya wanawake,mi hapa mjni nimekuja kutafuta maisha mambo ya wanawake siyajui na sitaki kuyajua" nikasema " Acha ushamba dogo,maisha yapo na mapenzi yapo na lazima vyote viende kwa pamoja" akasema kaka Pale pale ukazuka mjadala mkubwa juu ya swala la mimi kutojihusisha na wanawake ambao ulidumu kwa muda 
"Dogo shemeji yako anataka kuelekea Kitunda kuangalia mradi wake wa kuku naomba umpeleke" akasema kaka Sikuwa na jinsi ya kukwepa ila nilijua nitapata shida sana njiani Tuliondoka na gari kuelekea huko,na kweli njiani shemeji aliendelea na mambo yake ya kipuuzi. 
Tulipofika Banana tukapinda kushoto na kushika njia inayoelekea Kitunda na Machimbo Kati kati ya safari kuna sehemu nyumba za watu si nyingi hivyo ni peupe kiasi flani nikashangaa shemeji akidai nisimamishe gari " Vip shem? Mbona hatujafika?" nikauliza " Naomba kukuuliza swali? Hivi si wewe ni shabiki wa mpira?" akauliza " 
Ndiyo na hilo linahusikaje sasa na safari yetu?" nikajibu na swali juu " Eti kabla mechi haijaanza si lazima wachezaji wafanye mazoezi kiasi kwa ajili ya kupasha mwili ili wakiingia kwenye mechi wawe fiti?" akauliza " Ndiyo,sa unafikili utaingia kwenye mechi ukiwa hujapasha si utachemka" nikajibu bila kujua lengo lake " Basi na sisi pia hatuwezi kuingia kwenye mechi bila kupasha,nataka tupashe" akasema " Sijakwelewa kwa kweli" nikamjibu " 
Ni hivi,wiki ijayo namaanisha siku mbili kutoka leo kakako anasafir na tumeelewana tutakuwa na mechi moja ya kukata na shoka,sasa hatuwezi kucheza mechi bila kupasha misuli hivyo nataka tupashe sasa hivi,na isitoshe wewe ni kuku wa kienyeji,lazima nikuelekeze usije kuuliza maswali ya kipuuzi siku ya mechi" akasema.

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.