MOURINHO ASEMA HANA UHAKIKA WA KUWA MENEJA WA MANCHESTER UNITED

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa hana uhakikika wa kuwa meneja mpya wa Manchester United.
Mourinho ambaye alifutwa kazi na mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea mwezi Desemba mwaka 2015, takriban miezi 7 pekee baada ya kulinyakua kombe la ligi kuu ya Uingereza, amekuwa akihusishwa kurithi mikoba ya Van Gaal kutokana na Mholanzi huyo kupata msururu wa matokeo ya kutoridhisha ndani ya Manchester United.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Singapore, Mourinho aliulizwa na wanahabari iwapo ana mpango wa kumrithi kocha Louis van Gaal wa Manchester United
“Kwa hakika hilo ndilo swali kuu,” alisema Mourinho.
Aliongeza, “Hakuna ajuaye iwapo yale tunayoyasoma magazetini ni ya ukweli au la, hata mimi mwenyewe sijui,”
Mreno huyo hata hivyo anasema kuwa anamatumaini ya kurejea uwanjani msimu wa joto.
Mbali na Manchester United, Mourinho pia amehusishwa na klabu ya Serie A ya Italia Inter Milan mbali na mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid.
Post a Comment
Powered by Blogger.