MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA MJINI MH. COSATO CHUMI AINGILIA MVUTANO KATI YA WAMACHINGA NA HALMASHAURI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasikiliza wafanyabiasha wadogowadogo waliofika kueleza matatizo yao yanayowakabili kuhusu Halmashauri ya Mafinga.
  Wafanyabiasha wadogowadogo wakiwasikiliza Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi walipokutana naye walipokuja kutoa malalamiko yao.
NA FREDY MGUNDA, MAFINGA
Mvutano mkali kati ya wafanyabiashara wadogowadogo (machinga) mjini Mafinga mkoani Iringa na uongozi wa halmashauri hiyo umeendelea kufukuta baada ya wafanyabiashara hao kugomea kuondoka katika eneo hilo wakidai maslai ya watu wachache ndio yanayowahamisha katika eneo hilo jambo lilopelekea mbunge kuingilia kati  .

Wakitoa kilio chao mbele ya mbunge wa mafinga mjini Mh. Cosato Chumi wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na halmashauri hiyo  kwa kuhamishwa hamishwa kila kukicha na kupelekwa maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara zao .

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Glibet Amoni  alisema hapo awali walikuwa wakifanyia biashara zao bembeni ya soko la mafinga Uwanja wa mashuja na badaye kuja kuhamishwa katika eneo hilo na kupelekwa katika eneo la Kinyanambo ambalo pia halifai kwa biashara kwa kuwa kipindi cha mvua vitu vyao huzama kwenye maji kwa kuwa eneo hilo huwa linasimamisha maji pindi mvua inyeshapo .

Alisema kuwa baada ya kuona eneo hilo linaharibu biashara zao waliamua kurudi katika eneo lao la awali la mashuja na kuutaarifu uongozi wa halmashauri hiyo kuwa wamerejea katika eneo hilo  lakini walifanya biashara kwa majuma mawili na baadaye kuja kutangaziwa kuondoka katika eneo hilo na kwenda katika soko jipya ambalo pia miundombinu yake haijakamilika na wali sio eneo la wamachinga 

Alisema kuwa walishanga kusikia matangazo ya barabarani kuwa hakutakuwa na mnada katika eneo hilo siku ya jumapili na walipokwenda siku hiyo walikuta magari ya polisi yakiwa yametanda katika eneo hilo kuwazuiya kufanya biashara katika eneo hili jambo lililozidi kuwadhofisha kwa kuwa wengi wao wana mikopo katika maeneo mbalimbali na wanapaswa kurejesha mikopo hiyo

“Mh mbunge wewe ndio msaada wetu uliahidi kututetea sana tunaona kuna mambo ya siasa yanaingia hapa kwani huyu mwenyekiti wa halmashauri Charles Makoga anatulazimisha kwenda kule kwa kuwa yeye anavibanda vyake kule sokoni ndio mana analazimisha tupelekwe kule  na tushanga kuja kututangazia kibabe na kuondolewa na polisi kama vile ni majambazi wakati ushuru wao tunalipa na eneo huwa tunafanya usafi kwani wanatufanyia hivii au sisi sio watanzania ”

Waliongeza kuwa wao siku yao ya kufanya biashara ni siku moja tu ya wiki yani jumapili lakini wameshanga kuona uongozi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa soko kuu wanaolalamika kutokuuza bidhaa zao pindi mnada huo unapofanyika katika eneo jambo ambalo siyo la kweli.

Akipokea kilio cha wafanyabiashara hao mbunge huyo wa Mafinga mjini Mh. Cosato Chumi aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu ili kuweza kwenda kuzungumza na uongozi wa halmashauri hiyo ili kuona ni sababu gani zilizopelekea wao kutolewa katika eneo hilo na kupelekwa soko jipya eneo ambalo limetegwa kwa ajili ya soko na wala sio kwa ajili ya mnada wa siku moja .

Chumi alisema yeye kama mbunge hatokubali kuona wananchi wake wananyanyaswa na watu wachache kwani yeye ni mbunge wa watu wote na wala hatakubali kuona watu wake wakipelekwa katika maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara 

‘’Kilio chenu nimekisikia na mimi nataka kukimbizana na kasi ya Rais Magufuli ya kuwatetea wanyonge sioni sababu za msingi za nyie kuhamishiwa kule soko jipya wakati nyie huwa munafanya mnada siku moja tu hao wanaosema hawauzi kwanini wanakuwa wabinafsi hivyo wao wanauza siku sita nyie mnada wenu ni siku moja  halafu eti wanasemna hawauzi mi niwambie waache ubinafsi na hili sitakubaliana nao ’’

Chumi alisema kuwa kimahesabu kupeleka mnada katika eneo hilo lililojengwa kwa kwa ajili ya soko ni kupoteza mapato ya halmashauri kwani badala ya kukusanya ushuru wa siku saba kwa wiki watakuwa wanakusanya ushuru wa mnada ambao ni siku moja kwa wiki jambo ambalo kimahesabu halikubaliki 

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimsoni Mhagama alisema inapaswa busara kutumika katika kuwasimamia wafanyabiashara hao na kuchana na kutumia ubabe kwani nao wanahaki ya kufanyabiashara kama wanavyofanya watu wengine .

Mhagama alisema kuwa serekali ya Raisi Magufuli ni serekali inayowangalia wafanyabiashara wadogo kwa jicho la pili ili waweze kufanikiwa katika biashara hao na kuwanyanyasa au kuwahamisha bila ya kukaa chini na kukubaliaba siyo jambo la busra na ofisi yake atajaribu kuangallia jinsi gani ya kuwasaidia ili wafikie muafaka 
Post a Comment
Powered by Blogger.