MBARAKA YUSUPH AOKOA JAHAZI CCM KIRUMBA WAKATI TOTO AFRICANS IKITOKA SARE YA BAO 1-1 DHIDI KAGERA SUGAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Na Faustine Ruta, Mwanza
TIMU za Toto Africans na Kagera Sugar zimetoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo Toto Africans ilitangulia kufunga bao dakika ya 24 mfungaji akiwa Japhary Vedastus. 
Mfungaji alimalizia kazi nzuri ya Miraji Athumani kabla ya Kagera kusawazisha dakika ya 66 mfungaji akiwa Mbaraka Yusuph. Kikosi kilichoanza cha Timu ya Toto Africans cha Jijini Mwanza dhidi ya Kagera Sugar
Kikosi kilichoanza cha Kagera Sugar
Tayari kipute kuanzishwa
Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Toto Africans
Kipute kikiendelea ....patashika kwenye Lango la Timu ya Toto baada ya kupigwa kona kwenye mchezo wao Ligi Kuu Vodacom ambapo wameumaliza kwa sare ya bao 1-1.Baadhi ya Mashabiki walioingi CCM Kirumba 
Kipindi cha kwanza Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa vichwa chini baada ya kupigwa bao 1-0 na Toto ya hapa Jijini Mwanza
Wachezaji wa Kagera wakiwa hoi na huku wakijiuliza jinsi gani waweze kuikomesha Timu ya Toto kwenye Uwanja wao.Kocha wa Kagera Sugar Mohamed Richard maarufu kwa jina la Adolph akiwa kwenye wasiwasi baada ya Timu yake kuwa nyuma ya bao 1-0 katika kipindi cha kwanza bao lililofungwa dakika ya 24. Picha na Faustine RutaWachezaji wa Toto wakipongezana kwa baoKipindi cha pili Kocha aliwapa somo na wakaweza kutumia nafasi na kusawazisha bao hilo

Wachezaji wa Kagera Sugar walifanya mikakati na kuongeza bidii katika kipindi cha pili na kuweza kusawazisha bao.
Chupuchupu!!
Mbaraka Yusuph akipongezwa kwa bao la kusawazisha
Shangwe za kusawazisha bao!
Mbaraka Yusuph akipongezwa kwa bao la kusawazisha na wenzakeMchezaji wa Kagera Sugar akishangilia bao ambalo muda mchache lilikataliwa na Mwamuzi na kama si kukataliwa lingelikuwa la pili kwa Kagera.
Mh. Nassoro Amduni kutoka Kigoma(kushoto) ndie aliyekuwa Kamisaa wa Mtanange huo na kulia ni Bw. Malick Tibabimale Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba nae alikuwepo Uwanjani hapo kushuhudia kipute.
Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Kocha Mkuu wa Timu ya Kagera Sugar mara baada ya mechi kumalizika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Picha na Faustine RutaWaandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Kiongozi wa Timu ya Toto Africans mara baada ya mechi kumalizika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Post a Comment
Powered by Blogger.