MAWAZIRI WASISITIZWA KURUDISHA FOMU ZA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA KWA VIONGOZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. (Picha zote na Benedict Liwenga) 
Na. Immaculate Makilika.
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wasiorudisha   fomu za  Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu  wamesisitizwa kurudisha fomu hizo  leo kabla ya saa 12 jioni  katika  ya Ofisi ya Tume ya Maadili iliyopo jijini  Dar es salaam na watakaoshindwa kufanya hivyo watakua wamejitoa wenyewe kwenye nafasi zao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa ofisini kwake alipokutana na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah  Kairuki, ambapo ameeleza kuwa, kufuatia Semina  iliyofanyika Februari 25 mwaka huu kati yake na  Mawaziri kuhusu  Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu, ambapo Kamishna Mkuu, Mhe. Jaji Mstaafu Salome Kaganda alitoa maelezo kwamba kuna baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao hawajarudisha fomu hizo  hadi kufikia jana.

Akiwataja Viongzoi hao, Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Mawaziri ambao hawajarudisha fomu hizo ni akiwemo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. January Makamba, ambao wote hawajarudisha fomu za Rasilimali na Madeni na fomu za Ahadi ya Uadilifu, vilevile  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga ambaye  hajarudisha fomu ya Ahadi ya Uadilifu, na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, ambaye  hajarudisha fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni, pamoja na Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. Luhaga Mpina ambaye hajarudisha fomu zote mbili.

Mhe. Majaliwa, amewasisitiza Mawaziri hao kujaza fomu hizo kwa kua ni agizo la Mheshimwa Rais kujaza fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni, “viongozi watakaoshindwa  kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni  na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wanatakiwa kujieleza kwa kutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo na watachukuliwa hatua” alisema Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 9 Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma ya mwaka 1995 sura ya 8 inawataka viongozi wote wa umma   kujaza fomu za kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Tamko la Raslimali na Madeni) na fomu ya Ahadi ya Uadilifu mara wanapoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Lengo la kujaza fomu hizo ni kuwa na uwajibikaji kwa kiongozi juu ya uadilifu wake wakati wote anapokua mtumishi wa Umma.
Post a Comment
Powered by Blogger.