JOHN WOKA AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka, amefariki dunia alfajiri ya Jumanne hii.
Alikuwa akitibiwa katika hospitali hiyo baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi.
Woka amefariki baada ya juzi kupata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Post a Comment
Powered by Blogger.