HONGERA SHULE YA SEKONDARI KAIZIREGE ILIYOPO MKOA WA KAGERA KWA KUFAULISHA WOTE KWA KUPATA DARAJA LA KWANZA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Shule ya Sekondari ya Kaizerege ipo wilaya ya Bukoba Mjini, Mkoani Kagera na imechukua nafasi ya Kwanza Kimkoa na Nafasi ya Kwanza Kitaifa katika kategori ya Shule yenye wanafunzi wasiozidi 40.
Lazima nishangae vile Mungu anaweza fanya jambo la kushangaza katika akili za wanadamu. Mungu anaweza kuchukua kilicho kinyonge na kukitumia kuleta maajabu. Leo hii shule ambayo ilikuwa haifamiki na walio wengi, imeibuka na kuwa KIOO cha walio wengi kimkoa na kitaifa. 
Shule ya Kaizerege ilishika nafasi ya kwanza mwaka 2013 kwenye matokeo ya kidato cha nne kwa shule zilizokuwa na idadi ya wanafunzi chini ya 40, lakini mwaka jana ikaibuka tena kidedea ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Mwaka huu, wanafunzi wote 72 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza, isipokuwa mwanafunzi mmoja tu ambaye hakufanya mtihani.
“Siri ya mafanikio ni kuzingatia dira ya shule ambayo ni kutoa elimu bora,” alisema mkuu wa shule hiyo, Yona Ludonya.
“Pia jitihada za walimu kujitolea na kubobea katika masomo wanayofundisha kumechangia mafanikio haya.”
Kati ya wanafunzi 72 waliofanya mtihani huo na kupata daraja la kwanza, wahitimu tisa wamefaulu kwa kupata pointi saba, wakati 14 wamepata pointi nane na wengine 10 pointi tisa.

Kwa kupitia muujiza huu ninaomba na wewe ambaye ulikuwa unadhani hutafanikiwa kimaisha na kuwa milionea na dunia nzima kukujua na kukutambua, leo hii amini inawezekana na ukawa mtu wa ajabu sana duniani na ukashangaza walio wengi. Ila thamini kazi yako, heshimu kazi yako, iamini kazi yako ya kuwa itakuinua siku moja, fanya kazi kwa bidii kama punda.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Post a Comment
Powered by Blogger.