BALOZI PIERRE MUTAMBA AWATAKA WAKONGO KUFANYAKAZI KWA BIDII, AKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Balozi Pierre Mutemba (katikati) akiimba wimbo wa Taifa.Na Maria Inviolata
Balozi mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi  ya Kongo nchini Tanzania (DRC)  Pierre Mutamba amewataka Wakongomani waishio nchini Tanzania kuwa na umoja na kufanyakazi kwa bidii  ili waweze kujenga nchi yao, amesema hayo wakati  Balozi huyo akianza kazi rasmi, leo katika ofisi za Ubalozi huo zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.
Balozi Mutamba amewaambia wanajumuia hao kuwa falsafa yake ni “Ni hapa kazi tu” inayofuata nyayo za Kauli  Mbiu ya Rais John Pombe Magufuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Mutamba alitoa Bendera za Taifa lake kwa kila Kiongozi wa jumuia ya Wakongomani  waishio hapa nchini ikiwa ni ishara ya Uzalendo wa Taifa lao, Balozi huyo alisema kuwa Bendera ni Nembo  ya Nchi, kwa hiyo ni jukumu la kila Mkongomani kuijenga nchi yake.
Wakongomani waishio hapa nchini walimundalia Balozi Mutamba  hafra fupi ya kumkaribisha kufanya kazi hapa nchini, hafra hiyo  ilifanyika katika ofisi za Ubalozini huo. Viongozi wa jumuia mbalimbali za Wakongomani hao wamesifu uteuzi wa Rais Joseph Kabila wa  kumteua Balozi  Mutamba  hapa nchini,  kwani  uwakilishi wake umewapa matumaini, kwa jinsi Balozi huyo alivyochukua hatua ya haraka kufungua milango kwa Wakongo wote waishio hapa nchini ubalozini hapo kushirikiana naye kudumisha uhusiano wa nchi hiyo na Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii.

Naye Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Kongo (BCI) waishio hapa nchini Mukendi Kabobu amehaidi kuwa wafanyabiashara wa chama hicho watampa ushirikiano mkubwa Balozi huyo kuondoa kero zote zilizokuwa zikikwamisha shughuli zao. Rais wa chama  cha hicho cha wafanyabiashara, amesema kuwa chama hicho kinafanya kazi pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania na wengine wakiwa wanachama wa chama hicho.
Kabobu amesifu utendaji wa Rais John Magufuri kwa kurekebisha mambo mengi kwa kipindi kifupi cha uongozi wake. Mwenyekiti wa wazee wa Kikongomani hapa nchini amemfananisha  Balozi Pierre Mutamba na ‘Kichwa kizuri cha mashua’ ambaye atawavusha salama’ kwani Balozi huyo amekuja na falsafa ya kuwaunganisha pamoja Wakongo wote.
Post a Comment
Powered by Blogger.