TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawatangazia waombaji wote wa mikopo wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo kuwa mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ni tarehe 31 Julai, 2013 na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawasisitizia waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: www.olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti:www.heslb.go.tz kabla ya tarehe 31 Julai, 2013.

Kila mwombaji anakumbushwa kusoma kwa umakini mwongozo wa ujazaji wa fomu ya maombi ya mikopo kwa mwaka 2013/2014 na kulipia ada ya shilingi 30,000/= kwa waombaji wapya kwa njia ya M-Pesa.

Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Post a Comment
Powered by Blogger.