MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kikosi kazi cha kitaifa cha kutathmini Ikolojia ya Mto Ruaha Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Kikosi kazi cha kitaifa cha kutathmini Ikolojia ya Mto Ruaha kikiwa katika moja ya skimu za umwagiliaji Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Bunge, Ndg. Chacha Nyakega (aliesimama) akifafanua jambo wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha uongozi  wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (katikati) akiongoza kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma​.
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akizungumza na wanufaika wa maradi wa kuandika mawazo ya biashara ambao wapo hapa nchini juu ya namna watakvyoweza kushirikiana na Benki ya UBA katika kukuza biashra zao mpaka nje ya mipaka ya Tanzania
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi cheti kwa Hurbert  Mwashiuya juu kama mnufaika wa mradi mara baada ya kupata ruzuku.
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi  cheti kwa Bi , Aika Mtei kma mmoja wa wanufaika wa ruzuku mara baada ya kuandika mradi juu ya biashara katika mtandao
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwaeleza watendaji wa Benki ya UBA juu ya umuhimu wa kuwasaidia wanufaika hao hili waweze kuwa mfano kwa wengine
Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika na baadhi ya watendaji wa beki hiyo
Baadhi ya wananchi Wa Kara ya Olasiti kama wanavyoonekana  pichani.Picha na Vero Ignatus blog.

Na .Vero Ignatus,Arusha.
WAKAZI wa Olasiti jijini Arusha wamesusia maji yanayotolewa na Idara ya maji na kudai kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya aina yoyote.

Wakizungumza  katika mkutano wa hadhara uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wananchi hao walisema maji yaliyosambazwa na Idara ya maji yana  chumvi kiasi cha kuharibu  hata mimea wanapojaribu kumwagilia.

Mmoja wa wakazi hao Meck  Mollel alisema wanahofia baada ya miaka ijayo kutokuwa na nguvu za kiume kutokana na kuendelea kutumia maji hayo ambayo yanaladha ya magadi.

"Kweli haya maji yanatupa hofu baadaye tutajikuta wanawake wote kwa mpango huu hatuyahitaji haya maji tuleteeni maji yaliyorafiki kwa binadamu" alisema Mollel.

Naye mkazi  mwingine alisema maji hayo akiwapa vifaranga wanapata matege kutokana na hali ya chunvi iliyozidi ambapo pia alisema akimwagilia mimea inakuwa ya njano.

Hata hivyo mkuu wa mkoa aliwataka wananchi hao kufahamu kuwa serikali haiwezi  kuruhusu maji yasiyo faa kwa matumizi ya binadamu  hivyo maji hayo yalipimwa na kuonekana yanafaa ndio maana yakaruhusiwa.

"Serikali  yoyote duniani haiwezi  kuruhusu kitu chenye madhara kwa wananchi wake hivyo  tutaleta tena wataalamu  kuyapima  tena na majibu yatakayopatikana  tutajua cha kufanya" alisema Gambo.

Naye Mkurugenzi wa maji jiji la  Arusha Ruth Koya alisema  kiwango cha maji salama hakipimwi kwa macho  bali  kinapimwa maabara  hivyo wataalam wamepima na wakaona yanafaa kwa matumizi.

Koya alisema maji wanayolilia wananchi hao yanafloride lakini hayo yaliyopo pamoja na kuwa na chumvi hayana madhara kwa matumizi Kama wanavyolalamika wao..
Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maarufu cha NEXT DOOR kilichopo katika kitongoji hicho cha wastaarabu huwaka moto wa midundo ya aina mbalimbali inayoporomoshwa na IVORY BAND iliyosheheni vipaji visivyo vya kawaida. 

Ripota wa Globu ya Jamii alipotembelea hapo katika ukumbi wa NEXT DOOR Ijumaa hakuweza kuamini macho na masikio yake kukuta ukumbi umefurika mashabiki wakipata burudani toka kwa vijana hao. Akaamua kuhoji wahusika. 

“Bendi hii tulianzisha mwaka jana (2016) mwezi wa tano na wamiliki wake ni sisi wanamuziki wenyewe tukishirikiama na wenzetu kadhaa ambao tumewaajiri”, alisema mmoja wa wamiliki wa IVORY BAND, Rama Pentagone, wakati wa mapumziko mafupi. 
Pentagone, anayepiga kinanda, gitaa na kuimba alisema wamiliki wa bendi hiyo ni yeye, mwanamuziki mkongwe mwenye sauti tamu Saleh Kupaza, Omari Kisila na Amina Juma. “IVORY BAND bado hatujatoa mtindo wa kutumia kwa sababu sisi tunapiga muziki tofauti na wengie wengine, hasa ukizingatia kwamba hatupigi “Sebene”, alisema Pentagone. 

Saleh Kupaza aliyekuwa pembeni akipoza koo na maji alisema hatua ya kwanza ya kuanzisha bendi na kujiajiri wao wenyewe imefanikiwa kwa asilimia 100, na kwamba sasa wako katika hatua ya pili ambayo ni kuazalisha nyimbo kibao zenye mtazamo wa kitaiafa na kimataifa. 

“Malengo yetu ya mbeleni ni kuwa kundi la muziki la Kimataifa na endapo Mungu atatujalia kutimiza malengo yetu ni kufanya maonesho makubwa ndani na nje ya nchi”, alisema Kupaza. 


Omari Kisila akaongezea kwamba kwa kuwa inakaribia watimize mwaka mmoja toka waanze rasmi, IVORY BAND imepanga kufanya bonge la onesho litakaloandamana na sherehe za bendi hiyo kutimiza mwaka mmoja mnamo mwezi wa Julai. 

“Tumeamua kufanya onesho hilo kabambe mwezi wa Saba kwa sababu mwezi Mei na Juni utakuwa ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Mei na kumalizikia mwezi Juni”, alisema Kisila. 
Amesema ukumbi pamoja na tarehe rasmi ya kufanyika tukio hilo vitatangazwa muda utapokaribia, na kwamba kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kuanza kupasua anga za redio na TV kwa kutoa kibao chao cha utambulisho kiitwacho SHIKA MOYO unachokisikia hapo chini. Hicho ni moja ya vibao takriban kumi ambavyo husisimua mashabiki kila wapigapo.


Katika kuadhimisha wiki ya usalama na afya kazini mwaka 2017, Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) imefanya kongamano kwa kuwakutanisha kwa mara ya kwanza wadau wa OSHA nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.

Kongamano hilo limefanyika leo Alhamis Aprili 27,2017 katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi Stadi - VETA Moshi mkoani Kilimanjaro.
Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo ni kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia inayomiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ambao wamefuzu mafunzo mbalimbali ya usalama kazini yaliyotolewa na OSHA.
Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Hadija Mwenda alisema wanafarijika kuona jinsi makampuni ya uchimbaji madini nchini yalivyohamasika katika kuimarisha masuala ya afya na usalama kwenye maeneo ya kazi.
Mwenda alisema bado jamii inaamini kuwa masuala ya usalama mahali pa kazi ni ya watu wachache hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa makampuni ya uchimbaji madini ambao mbali na kuimarisha hali ya afya na usalama kazini pia wamejitokeza kwa wingi kuonesha kazi zao katika wiki ya afya na usalama kazini mwaka 2017.
“Watu wanadhani suala la usalama ni la wachache ndiyo maana hata washiriki wengi wa maonesho ya wiki ya usalama mahali pa kazi ni watu wa migodi,naomba jamii ielewe kuwa suala la afya na usalama ni la watu wote kwani tukizingatia usalama kazini tunajiepusha na magonjwa na vifo”,alieleza Mwenda.
“Ili kuonesha OSHA tunajali na kumuunga mkono rais John Pombe Magufuli katika suala la uchumi wa viwanda kwa mara ya kwanza tumekutana katika mkutano wa pamoja na wadau wetu ili tupate mrejesho wa nini taasisi zinafanya katika kuimarisha afya na usalama kazini kwa lengola kuboresha zaidi”,aliongeza Mwenda.
Akiwasilisha mada kuhusu namna mgodi wa Buzwagi unavyohakikisha kuna usalama mgodini,Afisa Usalama na afya wa mgodi huo Mustapha Mlewa alisema mgodi wao umeweka mstari wa mbele suala la afya na usalama kazini.
Alisema mgodi huo unatekeleza mradi wa Tunajali kwa kuwafundisha wafanyakazi wao namna ya kutambua vihatarishi, kujilinda wawapo mgodini lakini pia namna ya kutumia vifaa mbalimbali vya uokozi kwenye maeneo yao ya kazi.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akifungua kongamano la wadau wa Osha katika ukumbi wa VETA Mjini Moshi
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akielezea umuhimu wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuboresha mfumo wa afya na usalama mahali pa kazi
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akizungumza ukumbini
Maafisa kutoka mgodi wa dhahabu Buzwagi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda.Katikati ni Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akifuatiwa na afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa (kulia)
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akizungumza ukumbini
Maafisa kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakiwa ukumbini wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada kuhusu namna mgodi wa Buzwagi unavyozingatia masuala ya afya na usalama mgodini
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada kwenye kongamano la wadau wa OSHA katika ukumbi wa VETA Mjini Moshi
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada ukumbini 
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akielezea malengo ya mgodi huo kupitia mpango wa Tunajali / WE CARE
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akielezea namna wanavyojali wafanyakazi wao wawapo mgodini
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akitoa mada kwenye kongamano hilo
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko 
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.

 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. PICHA NA JOHN BANDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

John Banda, Dodoma

CHAMA cha Tanzania Girl Guides (TGGA) kimezindua mradi wa upandaji miti kitaifa katika Shule ya Msingi ya Mtumba Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides nchini, Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshaanza upandaji wa miti hiyo katika mikoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza

Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.

Naye Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa, Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Guides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika hilo zinafaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye rutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali   

 Wanachama wa Tanzania Girl Guides wakichimba moja ya mashimo ya kupanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba Manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti katika shule mbalimbali nchini.
 Wanafunzi wanachama wa TGGA
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya kabila la Wagogo wakati wa uzinduzi wa upandaji miti shuleni hapo
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika kitaifa shuleni hapo juzi.

 Mwenyekiti wa TGGA, Marha Qorro akimwagilia mti baada ya kuupanda

 Viongozi na wanachama wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja
 Viongozi wa TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma
 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa TGGA
Wanafunzi wanachama wa TGGA wakiwa na miche ili waendelee na zoezi la kupanda miti shuleni hapo.
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.